2 Wakorintho Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziIngawa inaonekana kwamba waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wakorintho uliwasaidia, bado mivutano na mashindano yalikuwa yakiendelea. Walimu wa uongo walikuwa wamejiingiza ndani ya kanisa, wakiwa wanapinga na hata kushambulia uadilifu wa Paulo mwenyewe, na mamlaka yake kama mtume. Wengine katika kanisa hawakutaka kutubu. Hivyo Paulo aliamua kutorudi huko hadi tabia zao zibadilike.Paulo aliandika waraka huu kueleza hisia zake kuhusu wajibu, shauku na majukumu katika ushirika wa Wakorintho, na pia kujibu mashambulizi yaliyokuwa yameelekezwa kwake binafsi kama mtume. Katika kushughulikia matatizo hayo, Paulo alithibitisha mamlaka yake kama mtume.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuthibitisha huduma ya Paulo, na kutetea uwezo wake kama mtume, na pia kuyakataa mafundisho ya uongo katika kanisa la Korintho.MahaliMakedonia.TareheMnamo 55–57 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Tito, Timotheo, na walimu wa uongo.Wazo KuuMaisha binafsi na utumishi wa Paulo: anaorodhesha mambo aliyoyapitia katika maisha yake kama mtumishi wa Kristo.Mambo MuhimuJinsi tunavyoweza kupata ushindi katika mateso, na jinsi neema ya Mungu inavyotenda kazi kuleta mema kutokana na mateso. Paulo pia anatetea utume wake na kuwaonya wasiotii.YaliyomoSalamu na utambulisho, faraja kwa Wakristo (1:1–2:17)Maelekezo kuhusu huduma ya kweli (3:1–6:2)Habari za Paulo mwenyewe (6:3–7:16)Neema ya utoaji na maelekezo kuhusu changizo (8:1–9:15)Utetezi wa Paulo kuhusu huduma yake (10:1–12:21)Maonyo ya mwisho, na salamu (13:1‑14).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help