Zaburi 150 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 150Msifuni Bwana

kwa ukuu wake

1Msifuni Bwana.

Msifuni Mungu katika patakatifu pake,

msifuni katika mbingu zake kuu.

2Msifuni kwa matendo yake makuu,

msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,

msifuni kwa kinubi na zeze,

4msifuni kwa matari na kucheza,

msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

5msifuni kwa matoazi yaliayo,

msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.

Msifuni Bwana!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help