Zaburi 141 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 141Maombi ya kuhifadhiwa dhidi ya uovuZaburi ya Daudi.

1Ee Bwana, ninakuita, njoo kwangu hima.

Sikia sauti yangu ninapokuita.

2Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba;

kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.

3Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu,

weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

4Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya,

nisije nikashiriki katika matendo maovu

pamoja na watu watendao mabaya,

wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.

5Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;

na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.

Kichwa changu hakitalikataa.

Hata hivyo, maombi yangu daima

ni kinyume cha watenda maovu.

6Watawala wao watatupwa chini

kutoka majabali,

waovu watajifunza kwamba maneno yangu

yalikuwa kweli.

7Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi,

ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.”

8Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi,

ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.

9Niepushe na mitego waliyonitegea,

kutokana na mitego iliyotegwa na watenda maovu.

10Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,

wakati mimi ninapita salama.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help