2 Samweli Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziKitabu cha 2 Samweli kinaendeleza historia ya kuanzishwa kwa ufalme katika Israeli. Kinaanza na kifo cha Sauli, na kuendelea na habari za kutawazwa kwa Daudi kuwa mfalme wa Israeli, na pia kipindi chote cha utawala wake. Kinaweka kumbukumbu ya vita na matukio mengine ya wakati wa utawala wa Daudi kama vile kutekwa kwa mji wa Yerusalemu (5:6‑16), dhambi ya Daudi na Bathsheba (11:1‑27), na uasi wa Absalomu (13:1‑20).MwandishiHajulikani kwa uhakika. Wengine wamesema inawezekana ikawa ni Zabudi, mwanawe Nathani; pia kitabu kina habari zilizoandikwa na Nathani na Gadi.KusudiKitabu hiki kinamwonesha Daudi kama mtu muhimu ambaye chini ya uongozi wake, taifa la Israeli lilifikia kilele cha umoja na nguvu kuliko nyakati nyingine zote katika historia yake.MahaliKatika nchi ya Israeli chini ya utawala wa Mfalme Daudi.TareheKama mwaka wa 930 K.K.Wahusika WakuuDaudi, Yoabu, Bathsheba, Nathani na Absalomu.Wazo KuuKitabu hiki kinaeleza kuhusu miaka arobaini ya utawala wa Mfalme Daudi, kikionesha jinsi ustawi wa watu wote kifamilia na kitaifa umefungwa katika hali ya kiroho na kimaadili ya kiongozi wao. Uadilifu au upotovu wa kiongozi huamua ustawi au kudidimia kwa jamii au taifa.Mambo MuhimuKukua kwa ufalme wa Israeli na utawala wa Mfalme Daudi.YaliyomoDaudi mfalme wa Yuda (1:1–4:12)Daudi aunganisha Israeli (5:1–24:25).