Kumbukumbu Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziKitabu hiki ndicho cha mwisho katika ule mgawanyo wa kwanza wa Agano la Kale ambao huitwa “Vitabu Vitano vya Sheria.” Katika hotuba zilizonakiliwa katika Kumbukumbu la Torati, Musa anafanya ufupisho wa dini ya Wayahudi kuwa Agano lililotolewa kwa baba zao. Hili Agano ndilo msingi wa uhusiano ulioanzishwa na Mungu baina yake na Waisraeli, wala si Sheria, ambayo sasa inadhihirishwa kwa Waisraeli kwa kuokolewa kutoka Misri na kutunzwa kwa muda wote wa kutangatanga huko jangwani. Baada ya miaka arobaini, Waisraeli walikuwa wamekaribia kuingia katika Nchi ya Ahadi. Lakini kabla ya kufanya hivyo, Musa alitaka kuwakumbusha historia yao, yaani yale yote ambayo Mungu alikuwa amewatendea, pamoja na amri zile zote walizopaswa kuendelea kutii kama taifa teule la Mungu.Mazungumzo ya kwanza ya Musa yalikuwa kuwakumbusha watu kuhusu wema wa Mungu kwa kipindi chote cha safari ili kuwapa nchi ya Kanaani. Mazungumzo ya pili yalikuwa ni muhtasari wa Sheria za Mungu zikiwepo Amri Kumi. Musa aliwaambia watu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa nguvu zako zote” (6:5) ili waweze kuendelea kuzifurahia baraka za Mungu. Pia Musa alitilia mkazo ukweli kwamba ili waweze kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, ilikuwa ni lazima watu wawafundishe watoto wao kumpenda Mungu na kuzitii amri zake. Kutokana na hilo, haki na uadilifu zingepenya katika maisha yao ya kila siku, kadiri ambavyo upendo wao ungeelekezwa kwa ndugu wa kiume na wa kike.MwandishiMusa, isipokuwa sura inayoeleza kuhusu kifo chake.KusudiKuwakumbusha Waisraeli kuhusu mambo yale Mungu alikuwa amewatendea, na kuwahimiza wajitoe kabisa kwake.MahaliMashariki mwa Mto Yordani, karibu na Yeriko, wakiwa wanaikabili nchi ya Kanaani.TareheMnamo 1407–1406 K.K.Wahusika WakuuMusa, Yoshua, na Waisraeli.Wazo KuuKitabu cha Kumbukumbu la Torati kinaishia kwa kuwakumbusha Waisraeli juu ya Agano ambalo Mungu alifanya nao (29), kuteuliwa kwa Yoshua kuwa kiongozi mpya (31), na kifo cha Musa (34).Mambo MuhimuIli kudumisha uhusiano wa upendo kati ya Waisraeli na Mungu, wazazi waliagizwa kuwafundisha watoto wao kumcha Mungu kwa kuwafundisha kwa kielelezo (4:9‑10; 6:7). Kwa kuadhimisha zile sikukuu za mwaka, yaani Pasaka, Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, Sikukuu ya Vibanda, Sikukuu ya Mavuno, pamoja na yale makusanyiko mengine, Waisraeli walivikumbusha vizazi vilivyofuata juu ya upendo wa Mungu uliooneshwa kwenye ukombozi wao kutolewa Misri na kuendelea kwao kutunzwa naye kwa kuwapa mazao.YaliyomoUtangulizi na mazungumzo ya kwanza ya Musa (1:1–4:43)Mazungumzo ya pili ya Musa (4:44–11:32)Sheria za maisha ya kila siku (12:1–26:19)Matokeo ya kutii na ya kutokutii (27:1–28:68)Kufanya upya agano (29:1–30:20)Baraka za Musa kwa Israeli, na kifo cha Musa (31:1–34:12).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help