1 Timotheo Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziNyaraka za 1 na 2 Timotheo na ule wa Tito zinatambuliwa kama nyaraka za kichungaji zilizoandikwa na Paulo. Alimwandikia Timotheo msaidizi wake, ambaye alikuwa amemwacha huko Efeso kusahihisha matatizo kadhaa kuhusu mwenendo wa kanisa, uongozi wa kanisa, na mambo yaliyowahusu waumini. Paulo aliandika ili kumpa Timotheo maagizo kuhusu mambo haya, ili kanisa lifanye kazi yake vyema. Aliandika pia kumtia moyo Timotheo asichoke katika maisha yake ya Kikristo, bali aishi maisha ya ukamilifu kwa utukufu wa Mungu.Timotheo alizaliwa huko Listra. Baba yake alikuwa Myunani, naye mama yake Myahudi ambaye alimfundisha Maandiko tangu utoto. Paulo alipofika Listra katika safari yake ya pili kueneza Injili, alimchagua Timotheo ambaye alishirikiana naye hadi mwisho wa huduma yake.MwandishiMtume Paulo.KusudiKumtia moyo na kumpa maelekezo Timotheo, ambaye alikuwa kiongozi mchanga, kuhusu utaratibu wa kanisa, imani na maadibisho.MahaliPengine Filipi.TareheMnamo 64 B.K.Wahusika WakuuPaulo na Timotheo.Wazo KuuUmuhimu wa kuwa na imani sahihi, mwenendo mnyofu, na pia uadilifu.Mambo MuhimuKumwelekeza Timotheo kuhusu sifa na wajibu wa viongozi mbalimbali katika kanisa, na kumpa mwongozo katika wajibu wake wa kichungaji.YaliyomoSalamu, na maonyo dhidi ya walimu wa uongo (1:1‑20)Maagizo kuhusu maombi (2:1‑15)Sifa zinazowapasa viongozi wa kanisa (3:1‑16)Maonyo na huduma (4:1–5:25)Huduma ya Kikristo, na maagizo kwa Timotheo (6:1‑21).