Ayubu Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziKitabu hiki kimepewa jina la mhusika wake mkuu ambaye ni Ayubu. Ayubu alikuwa ni mtu tajiri na mwenye haki mbele za Mungu. Maana ya jina Ayubu ni “Yule anayemrudia Mungu daima”. Hata baada ya kuondokewa na vitu vyote na kuugua majipu yaliyomletea maumivu na mateso makali mwilini, Ayubu bado alikiri kumpenda Mungu. Lakini rafiki zake Ayubu walisisitiza kwamba alikuwa anateseka kwa sababu alikuwa ametenda dhambi, na kwamba hiyo ilikuwa ni adhabu yake. Ayubu alijitetea kwa kusisitiza kwamba hajafanya uovu ambao ungemsababishia hiyo adhabu na kwamba yeye anamwamini Mungu. Ndipo Mungu alipozungumza na kuonesha uwezo wake mkubwa. Mwishowe, Ayubu alikiri kwamba Mungu ni mkuu na wa ajabu kwetu, kiasi kwamba hatuwezi kumwelewa.MwandishiHaijulikani kwa dhahiri ni nani aliyekiandika kitabu hiki; huenda ikawa ni Ayubu. Wengine hudhani ni Musa, Sulemani au Elihu.KusudiKitabu hiki kinaonesha mateso ya mwenye haki, uweza na uaminifu wa Mungu, na pia kinathibitisha maana ya imani ya kweli ya mtu wa Mungu. Kitabu hiki kinaonesha baraka zinazoambatana na ushindi baada ya majaribu. Kwa hiyo kazi ya majaribu ambayo Mungu anayaruhusu ni kututhibitisha katika imani. Kitabu hiki kinazungumzia swali hili: “Ni kwa nini wenye haki huteseka?”MahaliInadhaniwa kuwa kitabu cha Ayubu kiliandikwa katika nchi ya Usi. Nchi hii ilikuwa kaskazini mashariki mwa Palestina, karibu na jangwa lililo kati ya Dameski na Mto Frati.TareheTarehe ya kuandikwa kwa kitabu hiki haijulikani; kinadhaniwa kuwa kitabu cha zamani sana kuliko vingine vyote katika Biblia. Yawezekana kuwa mambo yalioandikwa kwenye kitabu hiki yalitukia mnamo 2000–1800 K.K.Wahusika WakuuAyubu, Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, Sofari Mnaamathi, na Elihu wa kabila la Buzi.Wazo KuuMungu ametuwekea ugo pande zote. Hivyo Shetani hawezi kutushambulia bila Mungu kujua, lakini wakati mwingine Mungu hutoa ruhusa ili kumthibitishia adui juu ya uelekevu na uadilifu wa mtu wake. Hivyo basi, kumtumaini Mungu wakati wote na katika hali zote huleta ushindi dhidi ya Shetani.Mambo MuhimuKujaribiwa kwa Ayubu, mazungumzo kati ya Ayubu na rafiki zake watatu, na majibu ya Mungu kwa Ayubu yaliyoambatana na baraka ya watoto na mali nyingi kwa Ayubu.YaliyomoSehemu ya kwanza: Habari za awali, na Ayubu kujaribiwa (1:1–2:13)Sehemu ya pili: Mazungumzo ya Ayubu na rafiki zake watatu (3:1–31:40)Mungu anahusikaje na mateso ya Ayubu? (3:1–14:22)Je, watu waovu huwa wanateseka mara zote? (15:1–21:34)Je, Ayubu ana hatia ya kuwa na dhambi ya siri? (22:1–31:40)Sehemu ya tatu: Mazungumzo ya Elihu (32:1–37:24)Sehemu ya nne: Bwana amjibu Ayubu (38:1–41:34)Sehemu ya tano: Ayubu amjibu Bwana, na Mwisho (42:1‑17).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help