Zaburi 149 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 149Wimbo wa kumsifu Mungu kwa wema wake

1Msifuni Bwana.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

2Israeli na washangilie katika Muumba wao,

watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.

3Na walisifu jina lake kwa kucheza

na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

4Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake,

anawavika wanyenyekevu taji la wokovu.

5Watakatifu washangilie katika heshima hii,

na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.

6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao

na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,

7ili walipize mataifa kisasi

na adhabu juu ya mataifa,

8wawafunge wafalme wao kwa minyororo,

wakuu wao kwa pingu za chuma,

9ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao.

Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote.

Msifuni Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help