Zaburi 124 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 124Shukrani kwa ukombozi wa IsraeliWimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Kama Bwana hangekuwa upande wetu;

Israeli na aseme sasa:

2kama Bwana hangekuwa upande wetu,

watu walipotushambulia,

3hasira yao ilipowaka dhidi yetu,

wangetumeza tukiwa hai,

4mafuriko yangegharikisha,

maji mengi yangetufunika,

5maji yaendayo kasi

yangetuchukua.

6Ahimidiwe Bwana,

ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.

7Tumeponyoka kama ndege

kutoka mtego wa mwindaji;

mtego umevunjika,

nasi tumeokoka.

8Msaada wetu ni katika jina la Bwana,

Muumba wa mbingu na dunia.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help