Zaburi 146 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 146Kumsifu Mungu mwokozi

1Msifuni Bwana!

Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,

2Nitamsifu Bwana maisha yangu yote;

nitamwimbia Mungu wangu sifa

wakati wote ningali hai.

3Usiweke tumaini lako kwa wakuu,

kwa wanadamu ambao hufa,

ambao hawawezi kuokoa.

4Roho yao itokapo hurudi mavumbini,

siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.

5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,

ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,

6Muumba wa mbingu na nchi,

na bahari na vyote vilivyomo:

Bwana anayedumu kuwa mwaminifu

milele na milele.

7Naye huwapatia haki waliodhulumiwa,

na kuwapa wenye njaa chakula.

Bwana huwaweka wafungwa huru,

8 Bwana huwafumbua vipofu macho,

Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao,

Bwana huwapenda wenye haki.

9 Bwana huwalinda wageni

na kuwategemeza yatima na wajane,

lakini hupinga njia za waovu.

10 Bwana atamiliki milele,

Mungu wako, ee Sayuni,

kwa vizazi vyote.

Msifuni Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help