2 Yohana Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziWaraka wa pili wa Yohana uliandikwa kwa mama mteule na watoto wake. Unaweza kuwa ulimhusu mtu binafsi na jamaa yake, au ulilihusu kanisa fulani. Msisitizo unawekwa katika umuhimu wa imani kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu katika umbo la mwanadamu. Inawapasa waumini wanaosoma kudumu katika pendo la Mungu, na kukataa mafundisho mapotovu yanayopinga imani ya kweli.Yohana pia aliandika kuwaonya ili waweze kutambua walimu wa uongo waliosafiri kila mahali, wasije wakawaunga mkono na kuwasaidia. Yaani mtu yeyote asije akachangia kwenye kueneza mafundisho ya uongo badala ya yale ya kweli.MwandishiMtume Yohana.KusudiKuhimiza mwenendo wa muumini, na maonyo kuhusu walimu wa uongo na mbinu zao.MahaliEfeso.TareheMnamo 90 B.K.Wahusika WakuuYohana, mama mteule na watoto wake.Wazo KuuMtume Yohana anaagiza watu kuenenda katika kweli na kumtii Mungu, wakijihadhari na walimu wa uongo, ili wapate kumpenda Mungu, na kupendana wao kwa wao.Mambo MuhimuPendo la kweli ni kuwajali wengine. Tunatamani kupendwa na kuwapenda wengine, lakini tunaona mifano michache sana ya uhalisi katika jambo hili. Dunia imejaa ubinafsi, uchoyo na kujipenda mwenyewe.YaliyomoSalamu (1‑3)Kweli na upendo (4‑11)Salamu za mwisho (12‑13).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help