Waefeso Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziPaulo aliandika waraka huu akiwa gerezani huko Rumi ili kuwatia moyo waumini wa jimbo la Asia. Waraka huu ulikuwa kama mwongozo uliokusudiwa kwa makanisa kadhaa. Zaidi ya hayo, kwenye waraka huu hakuna salamu za watu binafsi, wala hakuna matatizo maalum. Paulo alielezea kwamba kanisa lilianzishwa na Mungu, akiwaelezea mpango wa Mungu wa tangu awali wa kuwaokoa watu wake kupitia Kristo kwa imani. Mpango huu ulikuwako hata kabla ya ulimwengu kuumbwa. Mwenendo wa maisha mapya upo kinyume kabisa na ule wa maisha ya kale bila Kristo.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuwaimarisha waumini katika imani yao ya Kikristo kwa kueleza asili na kusudi la kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo.MahaliRumi.TareheMnamo 60 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Tikiko, na waumini wa Efeso.Wazo KuuMpango wa Mungu wa milele wa kuuokoa ulimwengu ulitimizwa kupitia kwa Kristo katika mwili wake.Mambo MuhimuUmoja katika Kristo na maisha mapya katika Kristo (2:4‑6), na umoja katika mwili wa Kristo. Pia maisha Wakristo wanayopaswa kuishi kuhusu ndoa, tabia, mwenendo, wazazi na watoto, watumishi na mabwana zao.YaliyomoMpango wa Mungu, na wokovu wa wote wanaomwamini (1:1–2:22)Siri ya Injili (3:1‑21)Maisha ya Mkristo duniani (4:1–6:9)Silaha za Mungu, salamu za mwisho (6:10‑24).