Danieli Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziKitabu hiki kinatoa kumbukumbu za Danieli wakati wa utumishi wake wa muda mrefu katika falme za Babeli na Uajemi. Alipokuwa mateka katika jumba la mfalme huko Babeli, Danieli alipandishwa cheo na kupewa wadhifa wa juu baada ya kumwambia Nebukadneza ndoto yake na fasiri yake. Katika mwongo wa mwisho wa maisha yake, Danieli alipata funuo kadha wa kadha kutoka kwa Mungu zilizowiana na ndoto ya Nebukadneza. Ndoto hizo zilionesha kuinuka na kuanguka kwa falme za dunia zilizostawi, ambazo hatimaye falme hizi zinafikia ukomo na Mungu anainua ufalme wa milele. Danieli, kama Myahudi mcha Mungu aliyekuwa mwombaji na msomaji wa Maandiko, alikuwa anawajali sana watu wake wa Israeli. Alihakikishiwa na Mungu kwamba wangefanywa imara tena.MwandishiDanieli.KusudiKueleza na kuonesha uweza wa Mungu kwamba ndiye anayetawala mbingu na nchi na kwamba falme zote za wanadamu ziko chini yake. Pia, kuonesha jinsi Mungu anavyoweza kuokoa wale wanaomtumaini.MahaliBabeli.TareheMnamo 536–530 K.K.Wahusika WakuuDanieli, Shadraki, Meshaki, Abednego, Nebukadneza, Belshaza na Dario.Wazo KuuUkuu wa Mungu ambaye anatawala historia yote.Mambo MuhimuMaono ya Danieli yanaonesha mpango wa Mungu kwa vizazi vyote, pamoja na kutabiri kuhusu ujio wa Masiya.YaliyomoDanieli na rafiki zake wahudumu chini ya wafalme wa Babeli (1:1–5:31)Danieli katika tundu la simba (6:1–6:28)Maono wakati wa utawala wa Belshaza (7:1–8:27)Ndoto ya Danieli na majuma sabini (9:1‑27)Maono ya mwisho ya Danieli (10:1–12:13).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help