Zaburi 93 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 93Mungu ni mkuu

1 Bwana anatawala, amejivika utukufu;

Bwana amejivika utukufu

tena amejivika nguvu.

Dunia imewekwa imara,

haitaondoshwa.

2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;

wewe umekuwa tangu milele.

3Bahari zimepaza, Ee Bwana,

bahari zimepaza sauti zake;

bahari zimepaza sauti za mawimbi yake.

4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,

ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:

Bwana aishiye juu sana ni mkuu.

5Ee Bwana, sheria zako ni imara;

utakatifu umepamba nyumba yako

pasipo mwisho.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help