Yoeli Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziYoeli mwana wa Pethueli maana ya jina lake ni “Bwana ni Mungu”. Nyingi ya kumbukumbu zake katika kitabu hiki na huduma yake hekaluni zinaonesha kwamba alikuwa nabii aliyetumwa kwa Yuda na Yerusalemu. Kutokana na huduma yake, wengi wamemdhania kuwa nabii wa “kikuhani” (linganisha Yer 28:1, 5) aliyenena neno la kweli la Bwana.Tukio hili lilitafsiriwa kuwa ni pigo kwa sababu ya dhambi za watu. Yoeli alilitafsiri tukio hili kuwa ni kielelezo cha ujio wa “siku ya Bwana”, yaani siku ya hukumu. Tukio hili la nzige lilileta maombolezo makubwa katika nchi ya Palestina na kupelekea makuhani kulia kilio kikuu. Hata hivyo, kitabu kinaonesha kuwa tukio la nzige halikuwa neno la mwisho kwani baada ya maombolezo makubwa, watu walifarijiwa kwa kuahidiwa kupata furaha kuu. Akiwaonya watu wamgeukie Bwana kwa toba, Yoeli anatangaza kwamba “siku ya Bwana” inakuja kwa ajili ya hukumu. Lakini Yoeli anaonesha kuwa kabla siku ya hukumu haijatimia, Mungu atatuma Roho wake ili kuleta baraka. Katika tukio la nzige, Yoeli aliona ishara ya hukumu ya mwisho, hivyo akawaonya watu watubu na kumrudia Mungu.MwandishiYoeli mwana wa Pethueli.KusudiKuonya Yuda juu ya hukumu ya Mungu iliyokuwa karibu kwa sababu ya dhambi zake; na kuwahimiza watu wamrudie Mungu.MahaliYerusalemu.TareheMnamo 835–796 K.K.Wahusika WakuuYoeli na watu wa Yuda.Wazo KuuHukumu na kumrudia Mungu.Mambo MuhimuPigo la nzige, kuwaonya watu watubu, na tumaini kwa watu wa Mungu.YaliyomoKuvamiwa na nzige (1:1–2:17)Maonyo na baraka za Mungu (2:18–3:12).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help