Zaburi 47 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 47Mtawala mwenye enzi yoteKwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

1Pigeni makofi, enyi mataifa yote,

mpigieni Mungu kelele za shangwe!

2Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana,

Mfalme mkuu juu ya dunia yote!

3Ametiisha mataifa chini yetu,

watu wengi chini ya miguu yetu.

4Alituchagulia urithi wetu,

fahari ya Yakobo, aliyempenda.

5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,

Bwana kwa sauti za tarumbeta.

6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,

mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.

7Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,

mwimbieni zaburi za sifa.

8Mungu anayatawala mataifa,

Mungu ameketi kwenye kiti chake cha enzi kitakatifu.

9Wakuu wa mataifa wanakusanyika

kama watu wa Mungu wa Abrahamu,

kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu;

yeye ametukuka sana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help