1 Petro Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziMtume Petro ni mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili wa Yesu. Aliandikia waraka huu kwa Wakristo wa Kiyahudi waliotawanyika huko sehemu ya Asia Ndogo. Waraka huu unaonesha kwamba waumini walikuwa wanakabiliwa na dhiki na mateso. Lengo lake lilikuwa kuwafariji waumini walioishi jimbo la Asia, kwani katika kipindi hiki cha miaka ya sitini ya karne ya kwanza, utawala wa Rumi chini ya Nero ulianza kuwatesa Wakristo.Kwa wale waliokuwa wakifikiria kurudia imani yao ya Kiyahudi ili kuepuka mateso, anawaambia kuwa sasa kanisa ndilo ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki yake Mungu. Hivyo mawazo ya kurejea imani ya Kiyahudi hayana faida yoyote. Kisha Petro anatoa mfano wa Kristo na jinsi alivyopata mateso, na anawakumbusha waumini kuwa wao pia hawana budi kupata mateso. Mwishowe, Petro anatoa maagizo kwa vikundi mbalimbali vya Wakristo.MwandishiMtume Petro.KusudiKuwatia moyo Wakristo kusimama dhabiti katika mateso yote, na kuwa imara katika neema ya Mungu.MahaliRumi.TareheMnamo 63 B.K.Wahusika WakuuPetro, Silvano, na Marko.Wazo KuuHata kama tutauawa kwa ajili ya imani, tushikilie imani yetu. Mungu anafahamu yote yanayotendeka, na katika mpango wake wa milele, hatimaye mambo yote yatakamilika kwa utukufu wake.Mambo MuhimuPetro anaonesha kwamba mateso ni sehemu ya maisha ya Kikristo, na kwamba Mungu ameandaa thawabu zisizoharibika kwa wote wanaomwamini. Pia anaonesha tumaini la wakati wa mwisho kuwa jambo la kumtia moyo muumini katika mateso.YaliyomoSalamu, utukufu wa wokovu wa Kristo (1:1‑25)Utiifu wa Mkristo (2:1‑25)Maisha yampasayo Mkristo (3:1–4:11)Huduma ya Kikristo, na salamu za mwisho (4:12–5:14).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help