Zaburi 142 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 142Maombi ya kuokolewa dhidi ya watesiUtenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Maombi.

1Namlilia Bwana kwa sauti,

napaza sauti yangu kwa Bwana anihurumie.

2Namimina malalamiko yangu mbele zake,

mbele zake naeleza shida zangu.

3Roho yangu inapozimia ndani yangu,

wewe ndiwe unajua njia zangu.

Katika njia ninayopita,

watu wameniwekea mtego.

4Tazama kuume kwangu na uone,

hakuna hata mmoja anayejihusisha nami.

Sina kimbilio,

hakuna anayejali maisha yangu.

5Ee Bwana, nakulilia wewe,

nasema, “Wewe ni kimbilio langu,

fungu langu katika nchi ya walio hai.”

6Sikiliza kilio changu,

kwa sababu mimi ni mhitaji sana;

niokoe na wale wanaonifuatilia,

kwa kuwa wamenizidi nguvu.

7Nifungue kutoka kifungo changu,

ili niweze kulisifu jina lako.

Ndipo wenye haki watanizunguka,

kwa sababu ya wema wako kwangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help