Zaburi 23 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 23 Bwana

mchungaji wetuZaburi ya Daudi.

1 Bwana ndiye mchungaji wangu,

sitapungukiwa na kitu.

2Hunilaza katika malisho

ya majani mabichi,

kando ya maji matulivu huniongoza,

3hunihuisha nafsi yangu.

Huniongoza katika njia za haki

kwa ajili ya jina lake.

4Hata nikipita katikati

ya bonde la uvuli wa mauti,

sitaogopa mabaya,

kwa maana wewe upo pamoja nami;

fimbo yako na mkongojo wako

vyanifariji.

5Waandaa meza mbele yangu

machoni pa adui zangu.

Umenipaka mafuta kichwani pangu,

kikombe changu kinafurika.

6Hakika wema na upendo vitanifuata

siku zote za maisha yangu,

nami nitakaa nyumbani mwa Bwana

milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help