2 Wathesalonike Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziWaraka huu uliandikwa miezi michache tu baada ya ule wa kwanza. Baadhi ya watu walikuwa wamemwelewa vibaya Paulo, au waraka mwingine wa bandia uliosemekana kuwa ulitoka kwa Paulo ulikuwa umewafadhaisha Wathesalonike kuhusu kurudi kwa Yesu. Paulo aliandika waraka huu ili kuwakumbusha yale aliyokuwa ametangulia kuwafundisha, akiwahakikishia waumini kuwa Kristo atarudi kuwafariji waliomwamini na kuwaadhibu wale waliokuwa wakiwatesa. Aliwaambia kwamba siku ya Bwana, yaani siku ya hukumu, haingewafikia mara moja, bali ingetanguliwa na matukio mbalimbali. Wakifahamu kuwa hakika Kristo angerudi, iliwapasa waumini kuishi maisha matakatifu yasiyo na lawama.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuondoa mkanganyiko kuhusu kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili.MahaliKorintho.TareheMnamo 51–52 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Silvano na Timotheo.Wazo KuuKuwafariji Wathesalonike kwa ajili ya mateso, na kuwahimiza waishi maisha ya kumtukuza Mungu.Mambo MuhimuKurudi kwa Yesu Kristo, na kuwaonya waumini wasiache kufanya kazi.YaliyomoFaraja kutokana na kurudi kwa Kristo (1:1‑12)Matukio kabla ya kuja kwa siku ya Bwana (2:1–3:5)Mausia ya Kikristo, na kuwatakia heri (3:6‑18).