Zaburi 85 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 85Maombi kwa ajili ya ustawi wa taifaKwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

1Ee Bwana, ulionesha wema kwa nchi yako.

Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.

2Ulisamehe uovu wa watu wako,

na kufunika dhambi zao zote.

3Uliweka kando ghadhabu yako yote

na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.

4Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena,

nawe uiondoe chuki yako juu yetu.

5Je, utatukasirikia milele?

Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?

6Je, hutatuhuisha tena,

ili watu wako wakufurahie?

7Utuoneshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana,

utupe wokovu wako.

8Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana;

anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake:

lakini nao wasirudie upumbavu.

9Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao,

ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.

10Upendo na uaminifu hukutana pamoja,

haki na amani hubusiana.

11Uaminifu huchipua kutoka nchi,

haki hutazama chini kutoka mbinguni.

12Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema,

nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.

13Haki itatangulia mbele yake

na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help