Zaburi 75 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 75Mungu ni mwamuziKwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu”. Zaburi ya Asafu. Wimbo.

1Ee Mungu, tunakushukuru,

tunakushukuru wewe,

kwa kuwa jina lako li karibu;

watu husimulia matendo yako ya ajabu.

2Unasema, “Ninachagua wakati maalum;

ni mimi nihukumuye kwa haki.

3Dunia inapotetemeka na watu wake wote,

ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

4Kwa wale wenye majivuno ninasema,

‘Msijisifu tena,’

kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

5Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;

msiseme kwa kiburi.’ ”

6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi

au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.

7Bali Mungu ndiye ahukumuye:

Humshusha huyu na kumkweza mwingine.

8Mkononi mwa Bwana kuna kikombe

kilichojaa mvinyo unaotoka povu

uliochanganywa na vikolezo;

huumimina, nao waovu wote wa dunia

hunywa hata tone la mwisho.

9Bali mimi, nitatangaza hili milele;

nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.

10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,

bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help