Zaburi 53 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 53Uovu wa wanadamu(Za 14)Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi.

1Mpumbavu anasema moyoni mwake,

“Hakuna Mungu.”

Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa,

hakuna hata mmoja atendaye mema.

2Mungu anawachungulia wanadamu chini

kutoka mbinguni

aone kama wako wenye akili,

wowote wanaomtafuta Mungu.

3Kila mmoja amegeukia mbali,

wameharibika wote pamoja,

hakuna atendaye mema.

Naam, hakuna hata mmoja!

4Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza:

wale ambao huwala watu wangu

kama watu walavyo mkate,

hao ambao hawamwiti Mungu?

5Hapo waliingiwa na hofu kuu,

ambapo hapakuwa na hofu.

Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia;

uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau.

6Laiti wokovu wa Israeli ungekuja kutoka Sayuni!

Mungu anaporejesha wafungwa wa watu wake,

Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help