Hosea 12 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

1Efraimu anajilisha upepo;

hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima

na kuzidisha uongo na jeuri.

Anafanya mkataba na Ashuru

na kutuma mafuta ya zeituni Misri.

2 Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda,

atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake

na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.

3Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake;

kama mwanadamu, alishindana na Mungu.

4Alishindana na malaika na kumshinda;

alilia na kuomba upendeleo wake.

Alimkuta huko Betheli

na kuzungumza naye huko:

5 Bwana Mungu wa majeshi,

Bwana ndilo jina lake!

6Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako;

dumisha upendo na haki,

nawe umngojee Mungu wako siku zote.

7Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu;

hupenda kupunja.

8Efraimu hujisifu akisema,

“Mimi ni tajiri sana; nimetajirika.

Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yangu

uovu wowote au dhambi.”

9“Mimi ndimi Bwana Mungu wenu

niliyewaleta kutoka Misri;

nitawafanya mkae tena kwenye mahema,

kama vile katika siku

za sikukuu zenu zilizoamriwa.

10Niliongea na manabii, nikawapa maono mengi

na kusema mifano kupitia wao.”

11Je, Gileadi si mwovu?

Watu wake hawafai kitu!

Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali?

Madhabahu zao zitakuwa

kama malundo ya mawe

katika shamba lililolimwa.

12Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu;

Israeli alitumika ili apate mke,

ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.

13 Bwana alimtumia nabii

kumpandisha Israeli kutoka Misri,

kupitia kwa nabii alimtunza.

14Lakini Efraimu amemchochea sana hasira;

Bwana wake ataleta juu yake

hatia yake ya kumwaga damu naye atamlipiza

kwa ajili ya dharau yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help