Filemoni Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziWaraka huu mfupi umeainishwa na nyaraka za Waefeso, Wakolosai na Wafilipi kama mojawapo wa nyaraka Paulo alizoandika akiwa gerezani. Aliandikia Filemoni na Afia, mwanamke Mkristo (ambaye huenda alikuwa mkewe Filemoni), na Arkipo, na kanisa lililokuwa likikusanyika nyumbani mwa Filemoni.Onesimo alikuwa mtumwa aliyetoroka kutoka kwa Filemoni huko Kolosai akaenda Rumi, ambako aliokoka. Onesimo, kama mtumwa, alikuwa mali ya Filemoni kisheria.MwandishiMtume Paulo.KusudiKumhimiza Filemoni amsamehe Onesimo, mtumwa aliyemtoroka, na amkubali kama ndugu Mkristo katika imani.MahaliRumi.TareheMnamo 60 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Filemoni, na Onesimo.Wazo KuuPaulo alimwandikia Filemoni kumshawishi amkubali Onesimo kurudi kwake, na amsamehe aliyomkosea.Mambo MuhimuBarua hii ni kielelezo cha ukarimu wa Kikristo. Paulo alishukuru kwa moyo wa ukarimu ambao tayari Filemoni alikuwa ameonesha kwa Wakristo wenzake. Paulo alikuwa na uwezo wa kumwamuru Filemoni, lakini alimwomba Filemoni ampokee Onesimo kwa upendo.YaliyomoSalamu (1‑3)Shukrani na maombi (4‑7)Paulo anamtetea Onesimo (8‑22)Salamu za mwisho (23‑25).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help