Zaburi 148 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 148Mwito kwa ulimwengu kumsifu Mungu

1Msifuni Bwana.

Msifuni Bwana kutoka mbinguni,

msifuni juu vileleni.

2Msifuni, enyi malaika wake wote,

msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.

3Msifuni yeye, enyi jua na mwezi,

msifuni yeye, enyi nyota zote zinazongʼaa.

4Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana,

na ninyi maji juu ya anga.

5Vilisifu jina la Bwana

kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.

6Aliviweka mahali pake milele na milele,

alitoa amri ambayo haibadiliki milele.

7Msifuni Bwana kutoka duniani,

ninyi wanyama wakubwa wa baharini,

na vilindi vyote vya bahari,

8miali ya radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu,

pepo za dhoruba zinazotimiza amri zake,

9ninyi milima na vilima vyote,

miti ya matunda na mierezi yote,

10wanyama pori na mifugo yote,

viumbe vidogo na ndege warukao,

11wafalme wa dunia na mataifa yote,

ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,

12vijana wa kiume na wanawali,

wazee na watoto.

13Wote na walisifu jina la Bwana,

kwa maana jina lake pekee limetukuka,

utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.

14Amewainulia watu wake pembe,

sifa ya watakatifu wake wote,

ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake.

Msifuni Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help