Mathayo Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziMathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye Bwana Yesu alimwita awe mwanafunzi wake hapo mwanzoni mwa huduma yake ya hadharani. Mathayo alianza kueleza kwa kirefu kuhusu Yesu alivyozaliwa na bikira Mariamu, alivyobatizwa, na kujaribiwa nyikani. Yesu alihubiri kuhusu ufalme wa Mungu, ambao ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika ufalme huu kwa kutubu dhambi na kumwamini Yesu. Mathayo aliyagawa mafundisho ya Yesu katika sehemu kuu tano: 1. Maadili, 2. Kueneza Habari Njema, 3. Mifano, 4. Ushirika, na 5. Kuja kwa ufalme wa Mungu. Sehemu ya mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza kuhusu kufa na kufufuka kwa Yesu, na agizo alilolitoa kwa wote wanaomwamini kueneza Habari Njema ulimwenguni kote.MwandishiMathayo aitwaye Lawi.KusudiKumtambulisha Yesu kwa Wayahudi kuwa ndiye Masiya, na pia Mfalme wa milele.MahaliPalestina.TareheMnamo 60–65 B.K.Wahusika WakuuYesu na wanafunzi wake, Mariamu, Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake, viongozi wa dini ya Kiyahudi, na Pilato.Wazo KuuKuthibitisha kwamba Bwana Yesu alikamilisha ahadi ambazo Mungu alitoa katika Agano la Kale.Mambo MuhimuKitabu hiki kinaelezea matukio manne ya maisha ya Yesu ya utotoni. Pia kinaelezea mifano kumi aliyoitoa Yesu, na miujiza miwili aliyoifanya. Ina midahalo tisa ambayo Yesu alihojiana na baadhi ya watu. Kinamalizia na hisia sita zilizoandamana na kusulubiwa kwake, na maagizo kwa wanafunzi wake kueneza Habari Njema duniani kote.YaliyomoMaisha na huduma ya awali ya Yesu (1:1–4:25)Mahubiri ya Mlimani (5:1–7:29)Mafundisho ya mifano na mazungumzo (8:1–18:35)Safari ya kwenda Yerusalemu, na maonyo ya mwisho (19:1–23:39)Unabii kuhusu mambo yajayo (24:1–25:46)Kufa na kufufuka kwa Yesu (26:1–28:20).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help