Wagalatia Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziPaulo aliandika waraka huu katika safari yake ya kwanza kueneza Injili. Baada yake kuondoka Galatia, waumini Wayahudi walifika huko, nao wakaanza kusisitiza kwamba lazima watu wa Mataifa walioamini kwanza watimize Sheria ya Musa ili wapate kuokoka. Paulo aliandika kupinga mafundisho hayo, akionesha jinsi Abrahamu, ambaye aliishi miaka 400 kabla ya Sheria ya Musa kutolewa, alivyookolewa kwa imani. Alionesha kwamba kama vile Sheria haingeweza kumwokoa mtu, basi hakuna mtu angeweza kuwa mkamilifu kwa kujitahidi kwa uwezo wake mwenyewe kuitimiza Sheria.MwandishiMtume Paulo.KusudiKukataa mafundisho ya kuwa muumini wa Mataifa ni lazima atii sheria za Kiyahudi ndio aokolewe.MahaliAntiokia.TareheMnamo 49 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Tito, Barnaba, Petro, na walimu wa uongo.Wazo KuuPaulo anatetea kwa bidii kweli ya Injili ambayo kiini chake ni kwamba, “Mtu anaokolewa kwa neema ya Mungu kwa kumwamini Kristo.”Mambo MuhimuPaulo anasisitiza uhalali wa Injili, ubora wa Injili, na uhuru wa Injili.YaliyomoPaulo atetea Injili na mamlaka yake kama mtume (1:1–2:21)Kuwekwa huru kutokana na Sheria (3:1–4:31)Uhuru wa Mkristo (5:1‑26)Mawaidha kuhusu mwenendo wa Mkristo (6:1‑18).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help