1 Wakorintho Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziKorintho ulikuwa mji uliojengwa pwani ya Mediterania (yaani Bahari Kuu). Mji huu ulistawi kwani ulikuwa kituo kikuu cha biashara. Ulikuwa koloni la Kirumi, ukiwavutia wakazi wa mataifa mbalimbali, wakiwemo Warumi, Wayunani na Wayahudi kutoka sehemu zilizoizunguka Bahari Kuu. Mchanganyiko huu wa wakazi ulisababisha kuharibika na kuzorota kwa maadili.Paulo alianzisha kanisa mjini Korintho katika safari yake ya pili kueneza Injili, na akakaa huko kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Aliondoka Korintho akifuatana na Prisila na Akila kwenda Efeso, na kutoka huko alitembelea kanisa la Yerusalemu, na baadaye akarudi Antiokia. Paulo alipokea habari kutoka kwa nyumba ya Kloe kwamba kanisa lilikuwa limegawanyika. Paulo aliona ni muhimu awaandikie waraka huu ili kujibu matatizo mengi yaliyojitokeza. Aliposhughulikia matatizo haya moja kwa moja, Paulo alifafanua misingi ya mafundisho ya Kikristo kuhusu imani na maadili.MwandishiMtume Paulo.KusudiKusahihisha makosa dhahiri katika kanisa la Korintho, na pia kuwaelimisha waumini jinsi ya kumtumikia Kristo katika jamii iliyokosa maadili.MahaliEfeso.TareheMnamo 55 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Timotheo, nyumba ya Kloe, waumini wa Korintho.Wazo KuuUmuhimu wa mwenendo wa Mkristo kufanana na Kristo.Mambo MuhimuSuluhu za matatizo mbalimbali kama: ugomvi kanisani, uzinzi, kushtakiana, mabishano juu ya ndoa, chakula kilichotolewa kwa sanamu, hali ya Paulo kuwa mtume, matumizi mabaya ya meza ya Bwana, ukweli kuhusu ufufuo, na mengine. Lazima mwenendo wa Mkristo ufanane na ule wa Kristo; kukosa kufanya hivyo ni kumwaibisha Kristo na kanisa lake.YaliyomoSalamu za Paulo (1:1‑9)Tatizo la mgawanyiko katika kanisa (1:10–4:21)Tatizo la zinaa katika kanisa (5:1‑13)Tatizo la kushtakiana mahakamani (6:1‑11)Tatizo la uasherati (6:12‑20)Tatizo kuhusu ndoa (7:1‑40)Matatizo kuhusu uhuru binafsi (8:1–11:16)Matatizo kuhusu meza ya Bwana na ibada (11:17–14:40)Matatizo kuhusu ufufuo wa wafu (15:1‑58)Mawaidha ya mwisho (16:1‑24).