Matendo Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziKitabu hiki ni cha pili katika vitabu viwili ambavyo Luka alimwandikia Theofilo. Kinajihusisha na huduma ya wafuasi wa Kristo. Luka anaonesha hali ambayo Kanisa la kwanza lilikabiliwa nayo wakati wa kuenea kwake katika utawala wa Rumi. Anathibitisha kuwa kazi ambayo Yesu alianzisha alipokuwa duniani, aliendelea kuifanya katika kanisa lake kupitia kwa Roho Mtakatifu. Katika kuenea kwa Ukristo, mkazo mkubwa uliwekwa kwa mitume kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.Petro ndiye anayeonekana sana wakati wa kuanzishwa kwa kanisa huko Yerusalemu. Tunaona jinsi kituo cha Ukristo kilihama hadi Antiokia ya Siria. Luka pia alionesha vile Paulo, ambaye alikuwa mtesi wa kanisa, hatimaye aliokoka na akawa kiongozi mkuu wa kanisa. Hivyo sehemu ya mwisho ya kitabu hiki imetoa nafasi kubwa kwa Paulo na utume wake. Kitabu kinaishia Paulo akiwa mfungwa anayehubiri Habari Njema huko Rumi.MwandishiLuka.KusudiKueleza utendaji wa Roho Mtakatifu na wa mitume katika kulithibitisha Neno la Mungu, na pia kutoa maelezo kuhusu kuanza kwa Ukristo, na jinsi Mungu alivyodhihirisha nafsi yake mwenyewe katika mwili wa Yesu Kristo kupitia kwa kanisa.MahaliHapajulikani.TareheMnamo 63–70 B.K.Wahusika WakuuPetro, Paulo, Stefano, Filipo na Barnaba.Wazo KuuKueleza jinsi Injili ilivyoenezwa kutoka kwa Wayahudi na kuwafikia watu wa mataifa mengine, na vile Injili ya kufa na kufufuka kwake Yesu ilivyo kiini cha msingi wa imani ya Ukristo.Mambo MuhimuKitabu hiki kinatoa kumbukumbu ya kuenea kwa Ukristo, kushuka kwa Roho Mtakatifu katika kanisa ili kuwatia mitume nguvu ya kuendeleza kazi ya Kristo. Kinaelezea jinsi Habari Njema ya Kristo ilivyoenea katika utawala wa Rumi, kuanzia Yerusalemu hadi Rumi.YaliyomoKanisa la kwanza (1:1–5:42)Mateso na kuenea kwa Injili (6:1–9:31)Matendo ya Petro (9:32–12:25)Safari ya kwanza ya Paulo kueneza Injili (13:1–14:28)Baraza la Yerusalemu na matokeo yake (15:1‑35)Safari ya pili ya Paulo kueneza Injili (15:36–18:22)Safari ya tatu ya Paulo kueneza Injili (18:23–21:16)Kukamatwa kwa Paulo na safari yake kwenda Rumi (21:17–28:31).