Zaburi 123 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 123Kuomba rehemaWimbo wa kwenda juu.

1Ninayainua macho yangu kwako,

kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi.

2Kama vile macho ya watumwa

yatazamavyo mkono wa bwana wao,

kama vile macho ya mjakazi

yatazamavyo mkono wa bibi yake,

ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu,

hadi atakapotuhurumia.

3Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu,

kwa maana tumevumilia dharau nyingi.

4Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi,

dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help