1Ee Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi!
Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!
2Wengi wanasema juu yangu,
“Mungu hatamwokoa.”
3Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao yangu pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
4Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.
5Ninajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.
6Sitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.
7Ee Bwana, amka!
Niokoe, Ee Mungu wangu!
Wapige adui zangu wote kwenye taya,
vunja meno ya waovu.
8Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana.
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.