Esta Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziKitabu hiki kinachukua jina la mhusika mkuu, ambaye ni Esta. Jina hili limetokana na neno la Kiajemi ambalo maana yake ni “Nyota.” Jina la Esta la Kiebrania ni “Hadassah,” maana yake “Mhadasi” ambayo ni aina ya miti iliyokuwa inastawi milimani karibu na Yerusalemu, na ilikuwa inatumika kujengea vibanda wakati wa Sikukuu ya Vibanda. Kitabu hiki kinaeleza kuhusu kisa cha msichana mzuri wa Kiyahudi ambaye Mfalme Ahasuero wa Kwanza alimchagua awe malkia wake.Matukio yaliyowapata Wayahudi yanayoelezwa kwenye kitabu hiki yalitokea huko Shushani, uliokuwa mji mkuu wa Uajemi chini ya utawala wa Mfalme Ahasuero aliyetawala Uajemi mnamo 486–465 K.K. Kule kuokolewa kwa Wayahudi kwa ajabu wakati wa Mfalme Ahasuero baadaye kuliadhimishwa kila mwaka kama Sikukuu ya Puri. Wakati huu, kitabu cha Esta husomwa hadharani.MwandishiMwandishi hajulikani, lakini inadhaniwa alikuwa ni Mordekai. Wengine hudhani ni Ezra au Nehemia kwa sababu ya mtindo wa kuandika.KusudiKuonesha ukuu wa Mungu, na upendo wake kwa watu wake.MahaliKatika jumba la kifalme huko Shushani, mji mkuu wa Uajemi.TareheKama mwaka wa 470 K.K.Wahusika WakuuEsta, Mordekai, Mfalme Ahasuero, na Hamani.Wazo KuuMungu aliwaokoa Wayahudi katika maangamizi yaliyopangwa na Hamani. Mungu aligeuza mabaya yaliyokusudiwa dhidi ya Wayahudi yakawapata adui zao katika utawala wote wa Mfalme Ahasuero, baada ya Esta na watu wake kumwomba Mungu.Mambo MuhimuEsta kuchaguliwa kuwa malkia badala ya Vashti aliyekuwa malkia kabla yake, na jinsi Mungu alivyobadilisha makusudi ya Hamani dhidi ya Wayahudi.YaliyomoEsta afanywa malkia (1:1–2:23)Hamani, Mordekai na Esta (3:1–7:10)Ushindi wa Wayahudi (8:1–10:3).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help