Zaburi 12 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 12Kuomba msaadaKwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.

1 Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;

waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.

2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;

midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

3 Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila

na kila ulimi uliojaa majivuno,

4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;

midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”

5“Kwa sababu wanyonge wanaonewa,

na wahitaji wanalia kwa uchungu,

nitainuka sasa,” asema Bwana.

“Nitawalinda kutokana na wale

wenye nia mbaya juu yao.”

6Maneno ya Bwana ni safi,

kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,

iliyosafishwa mara saba.

7Ee Bwana, utatuweka salama

na kutulinda na kizazi hiki milele.

8Watu waovu huenda wakiringa kila mahali

wakati yule aliye mbaya sana

ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help