Hosea 6 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Israeli asiye tubu

1“Njooni, tumrudie Bwana.

Ameturarua vipande vipande

lakini atatuponya;

ametujeruhi lakini

atatufunga majeraha yetu.

2Baada ya siku mbili atatufufua;

katika siku ya tatu atatuinua,

ili tuweze kuishi mbele zake.

3Tumkubali Bwana,

tukaze kumkubali yeye.

Kutokea kwake ni hakika kama vile

kuchomoza kwa jua;

atatujia kama mvua za masika,

kama vile mvua za vuli

ziinyweshavyo nchi.”

4“Nifanye nini nawe, Efraimu?

Nifanye nini nawe, Yuda?

Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,

kama umande wa alfajiri utowekao.

5Kwa hiyo nimewakata ninyi vipande vipande

nikitumia manabii wangu;

nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,

hukumu zangu zinawaka

kama umeme juu yenu.

6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,

na kumkubali Mungu

kuliko sadaka za kuteketezwa.

7Wamevunja agano kama Adamu:

hawakuwa waaminifu kwangu huko.

8Gileadi ni mji wa watenda maovu,

umetiwa madoa kwa nyayo za damu.

9Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu,

ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;

wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,

wakifanya uhalifu wa aibu.

10Nimeona jambo la kutisha

katika nyumba ya Israeli.

Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba

na Israeli amenajisika.

11“Pia kwa ajili yako, Yuda,

mavuno yameamriwa.

“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help