Waebrania Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziWaraka kwa Waebrania unajulikana kama kitabu cha mambo yaliyo bora, kwa sababu unazungumzia ukuu wa Kristo na kumdhihirisha kama ufunuo wa mwisho wa Mungu. Unabii na ahadi zilizoandikwa katika Agano la Kale zimetimizwa katika Agano Jipya, Kristo akiwa Mpatanishi. Kristo pia athibitishwa kuwa mkuu zaidi ya manabii, malaika, na Musa (ambaye alikuwa mpatanishi wa agano la hapo awali).Msomaji ameonywa asidharau wala kukataa wokovu mkuu uliotolewa kupitia kwake Kristo. Uwezekano mkubwa ni kwamba waraka huu ulielekezwa kwa Wakristo Wayahudi huko Palestina au Rumi, waliokuwa wanajaribiwa kugeukia tena dini ya Kiyahudi, au kuifanya Injili iwe yenye mfumo wa dini ya Kiyahudi.MwandishiIngawa waraka hauna jina la mwandishi, una ushahidi mwingi kwamba alikuwa mtu wa kizazi cha pili cha Wakristo aliyekuwa na ujuzi sana wa Agano la Kale.KusudiMwandishi anamwonesha Yesu kuwa ndiye ukamilifu wa ufunuo ulionenwa kwanza na Mungu, na kisha na manabii wake.MahaliRumi.TareheKabla ya kuharibiwa kwa Hekalu huko Yerusalemu mnamo 70 B.K.Wahusika WakuuYesu, Yoshua, Musa, Melkizedeki, Abrahamu, makuhani, malaika, na watu wenye imani wa Agano la Kale.Wazo KuuKiini cha Waebrania ni mamlaka na uweza wa Yesu Kristo kama Mjumbe wa neema ya Mungu. Kitabu hiki kinatoa sifa za majina ya heshima zaidi ya ishirini yaliyomtaja Yesu Kristo katika huduma ya ukuhani na ya ufalme.Mambo MuhimuYesu Kristo ni mngʼao wa utukufu wa Mungu, na pia Kristo ni mkuu kuliko malaika, mkuu kuliko viongozi wote, na mkuu kuliko makuhani.YaliyomoMnenaji bora kwa ajili ya Mungu (1:1–4:13)Mwombezi au Kuhani aliye bora (4:14–7:28)Agano jipya na Dhabihu iliyo bora (8:1–10:18)Wito wa kuitunza na kuilinda imani (10:19–12:29)Kanuni za maisha ya Kikristo, na maelezo ya binafsi (13:1‑25).