2 Petro Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziBarua hii inagusia matatizo ambayo Petro aliona yangetukia baada ya kifo chake. Aliwahimiza waumini waendelee kuijua kweli iliyo katika Injili ya Kristo. Kweli hii haikutokana na hadithi za kale, bali ilitokana na mambo waliyoyaona kwa macho. Aliwaonya kuhusu walimu wa uongo ambao wangetukuza mawazo yao wenyewe, badala ya mafundisho ya kweli ya Neno la Mungu. Hatimaye aliwakumbusha waumini kwamba Kristo atakuja siku moja kuangamiza hali ya asili ya ulimwengu huu.MwandishiMtume Petro.KusudiKuwaonya Wakristo kuhusu walimu wa uongo wanaojiingiza ndani ya kanisa, na kuwahimiza kukua katika imani yao na katika kumjua Kristo.MahaliUwezekano mkubwa ni kwamba waraka huu uliandikiwa Rumi.TareheMnamo 67 B.K.Wahusika WakuuPetro na Paulo.Wazo KuuUmuhimu wa kusimama imara katika imani, hata kukiwa na mafundisho mengi ya kupotosha.Mambo MuhimuPetro anashuhudia kwamba Mungu anataka watu waishi maisha matakatifu kwa ajili ya kukua katika kumcha Kristo. Juu ya yote, anataka wasomaji wake kukaza macho yao katika kuijua kweli ambayo inapatikana tu kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Kwa kumjua yeye, waumini wanapokea neema, amani, na mambo yote yapasayo uzima, na utauwa au kumcha Mungu.YaliyomoNamna ya kukua kiroho (1:1‑21)Maonyo kuhusu walimu wa uongo (2:1‑22)Siku ya Bwana (3:1‑18).