Zaburi 67 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 67Mataifa wahimizwa kumsifu MunguKwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo.

1Mungu aturehemu na kutubariki,

na kutuangazia nuru za uso wake,

2ili njia zako zijulikane duniani,

wokovu wako katikati ya mataifa yote.

3Ee Mungu, mataifa na wakusifu,

mataifa yote na wakusifu.

4Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe,

kwa kuwa unatawala watu kwa haki

na kuongoza mataifa ya dunia.

5Ee Mungu, mataifa na wakusifu,

mataifa yote na wakusifu.

6Ndipo nchi itatoa mazao yake,

naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

7Mungu atatubariki

na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help