Wafilipi Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziPaulo alitembelea mji wa Filipi katika safari yake ya pili kueneza Injili, kutokana na maono aliyoyapata akiwa Troa kumwelezea aelekee Makedonia. Filipi hapakuwa na Sinagogi kwa sababu ya idadi ndogo ya Wayahudi. Kanisa la Filipi lilimpelekea Paulo msaada kupitia kwa Epafrodito. Pia alitumia nafasi hiyo kuelezea matatizo aliyopata huko Rumi. Waumini wote waliambiwa wawe na malengo ya juu kabisa katika maisha yao ya Kikristo, kwa maana Mungu angewatimizia mahitaji yao yote katika maisha. Paulo aliwahimiza kufurahi nyakati zote.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuwashukuru rafiki zake wapendwa waliokuwa wamempelekea msaada kwa ajili ya mahitaji yake. Kuwatia Wafilipi moyo na kuwataka kusimama imara, akiwahimiza wawe na unyenyekevu kama aliokuwa nao Kristo, na pia wawe na umoja.MahaliRumi.TareheMnamo 61 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Timotheo, Epafrodito, Euodia na Sintike.Wazo KuuPaulo alisisitiza kuhusu furaha ya muumini katika Kristo.Mambo MuhimuPaulo anaagiza waumini kukataa kabisa mafundisho ya uongo na kuwahimiza wafurahi nyakati zote.YaliyomoPaulo na matatizo yake huko Rumi (1:1‑30)Kumwiga Kristo (2:1‑30)Mafundisho kuhusu mwenendo wa Mkristo (3:1‑21)Mausia, shukrani na salamu za mwisho (4:1‑23).