Zaburi 113 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 113Kumsifu Bwana

kwa wema wake

1Msifuni Bwana.

Enyi watumishi wa Bwana msifuni,

lisifuni jina la Bwana.

2Jina la Bwana na lisifiwe,

sasa na hata milele.

3Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,

jina la Bwana linapaswa kusifiwa.

4 Bwana ametukuka juu ya mataifa yote,

utukufu wake juu ya mbingu.

5Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu,

Yule aliyeketi kwenye kiti cha enzi huko juu,

6ambaye huinama atazame chini

aone mbingu na nchi?

7Huwainua maskini kutoka mavumbini,

na kuwanyanyua wahitaji

kutoka lundo la majivu,

8huwaketisha pamoja na wakuu,

pamoja na wakuu wa watu wake.

9Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,

akiwa mama watoto mwenye furaha.

Msifuni Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help