Zaburi 98 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 98Mungu Mtawala wa duniaZaburi.

1Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

kwa maana ametenda mambo ya ajabu;

kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu

umemfanyia wokovu.

2 Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane

na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.

3Ameukumbuka upendo wake

na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;

miisho yote ya dunia imeuona

wokovu wa Mungu wetu.

4Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote,

ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

5mwimbieni Bwana kwa kinubi,

kwa kinubi na sauti za kuimba,

6kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:

shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme.

7Bahari na ivume na kila kilicho ndani yake,

dunia na wote wanaoishi ndani yake.

8Mito na ipige makofi,

milima na iimbe pamoja kwa furaha,

9vyote na viimbe mbele za Bwana,

kwa maana yuaja kuhukumu dunia.

Atahukumu dunia kwa haki

na mataifa kwa haki.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help