Yona Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziJina Yona maana yake ni “Hua”. Kitabu hiki kinaelezea yale yaliyomtokea Yona kama mjumbe wa Mungu. Yona alikuwa ameagizwa na Mungu aende kuwaonya watu wa Ninawi juu ya hukumu iliyokuwa inakuja. Alijaribu kumkimbia Mungu na kuelekea Tarshishi, upande wa magharibi wa Israeli badala ya kuelekea Ninawi iliyokuwa kaskazini mashariki. Yona alitupwa baharini akamezwa na samaki mkubwa sana ambaye alimtapika pwani ya mashariki mwa Bahari ya Kati (Mediterania). Hatimaye alikwenda Ninawi na kuwaonya watu kuhusu hukumu ya Mungu na watu wa Ninawi walitubu. Badala ya kufurahia jambo hili, Yona alihuzunika na kuvunjika moyo kwa sababu Mungu alionesha rehema na kughairi hukumu dhidi ya watu wa Ninawi.MwandishiYona mwana wa Amitai.KusudiKuonesha ukuu wa rehema za Mungu na wokovu kwa mwanadamu. Pia, kuonesha jinsi ambavyo mwanadamu hawezi kukimbia wito wa Mungu.MahaliInaweza kuwa Israeli au Ninawi.TareheInadhaniwa kuwa mnamo 785–760 K.K.Wahusika WakuuYona, nahodha wa meli na mabaharia, mfalme wa Ninawi, na Waninawi wote.Wazo KuuUkuu wa rehema za Mungu.Mambo MuhimuRehema za Mungu na upendo wa Mungu kwa watu wote.YaliyomoYona amkimbia Mungu (1:1‑17)Maombi ya Yona na kuokolewa (2:1‑10).Yona aenda Ninawi (3:1‑10)Hasira ya Yona kwa ajili ya huruma ya Bwana (4:1‑11).