1 Wathesalonike Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziPaulo katika safari yake ya pili kueneza Injili alitembelea mji wa Thesalonike, ambao ulikuwa kituo cha biashara. Alihudumu huko kwa majuma matatu, akahubiri katika sinagogi la Wayahudi, akithibitisha kutoka Maandiko ya Agano la Kale kwamba Yesu ndiye Kristo. Baadhi ya Wayahudi na Wayunani wakaamini, lakini ilimlazimu Paulo kuondoka huko haraka kwa sababu ya upinzani mkubwa uliozuka humo.Baada ya kufika Athene, Paulo alipata habari kutoka kwa Timotheo kuwa ingawa walipata mateso, waumini wa Thesalonike walikuwa wamesimama imara. Paulo aliandika barua hii ili kuwatia moyo na kuwafariji waumini waliokuwa wachanga katika Kristo. Aliwaandikia ili kuimarisha imani yao kuhusu maisha yale Mkristo anapaswa kuishi, na pia kuhusu kurudi kwa Yesu. Yamkini waumini hawa walikuwa na wasiwasi kwamba Wakristo wenzao waliokuwa wamekufa hawangeweza kuufikia ufufuo wa wafu. Hivyo Paulo akawaandikia kuwahakikishia kwamba waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuwaimarisha Wakristo wa Thesalonike katika imani yao, na kuwapa hakikisho kuhusu kurudi kwa Yesu.MahaliKorintho.TareheMnamo 51 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Timotheo na Silvano.Wazo KuuKuwatia waumini moyo kudumu katika utakatifu, na kuwahakikishia wale wanaoteswa kwamba Mungu yu pamoja nao na amewaahidi ushindi.Mambo MuhimuPaulo aliwaandikia Wathesalonike barua hii ili kuwatia moyo na kuwafariji katika Kristo, na pia kuimarisha imani yao katika misingi ya mafundisho ya Kristo.YaliyomoSalamu na shukrani za Paulo (1:1‑10)Huduma ya Paulo Thesalonike, na matukio tangu kuondoka Thesalonike (2:1–3:13)Mwenendo na maisha ya kumcha Mungu (4:1‑12)Kurudi kwake Bwana Yesu (4:13–5:11)Maagizo ya mwisho, na hitimisho (5:12‑28).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help