Warumi Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziPaulo aliwaandikia watakatifu huko Rumi waraka huu. Wengi wa waumini wa kanisa hili walikuwa ni watu wa Mataifa. Paulo anaanza kwa kueleza kwamba wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Kwa hiyo Wayahudi na watu wa Mataifa hawawezi kudai haki mbele za Mungu, kwa sababu dhambi zao zinafuta haki hiyo. Lakini Mungu, kwa neema yake, anatuhesabia haki tuliyoipoteza kwa dhambi, haki tunayoipata kupitia kwa kumwamini Mwanawe, Yesu Kristo. Kwa njia hii ya kuhesabiwa haki na Mungu katika Mwanawe, tunaweza kuwa washindi katika maisha ya Kikristo. Kisha Paulo anaeleza nafasi ya Wayahudi katika mpango wa Mungu. Anamalizia waraka wake kwa kutoa maonyo kadha wa kadha kuhusu maadili.MwandishiMtume Paulo.KusudiPaulo kujitambulisha kwa kanisa la Rumi kwa ajili ya maandalizi ya safari yake, na pia ili kueleza kwa muhtasari msingi wa mafundisho yake.MahaliKorintho.TareheMnamo 57 B.K.Wahusika WakuuMtume Paulo, na waumini wa Rumi.Wazo KuuMpango wa Mungu wa wokovu na haki kwa wanadamu, kwa Wayahudi na pia watu wa Mataifa, kwa kuwa wote ni wenye dhambi (1:16‑17).Mambo MuhimuUfunuo kuhusu adhabu ya Mungu dhidi ya dhambi, na haki ipatikanayo kupitia kwa imani kama msingi wa kuhesabiwa haki.YaliyomoUtangulizi (1:1‑17)Watu wote hawana haki (1:18–3:20)Haki ipatikanayo kwa kumwamini Kristo (3:21–5:21)Kushinda dhambi kwa uwezo wa Kristo (6:1–8:39)Mpango wa Mungu kwa Israeli (9:1–11:36)Misingi ya maisha ya Kikristo (12:1–15:13)Mipango ya Paulo na mawaidha ya mwisho (15:14–16:27).