1 Yohana Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziWasomi wa waraka huu walikumbwa na mafundisho hatari sana ya Wanostiki, waliofundisha kuwa kila kitu kilikuwa kiovu, isipokuwa roho pekee ndiyo nzuri. Kati ya mafundisho yao, walikana misingi ya imani ya Kikristo kama vile: hali ya Kristo kuja katika mwili, mamlaka ya amri ya Kristo, hali ya mwanadamu kuwa mwenye dhambi, na wokovu kuwa ni kazi ya Kristo.Mwandishi wa waraka huu aligundua ya kuwa jamii ya waumini ilikuwa katika hatari kubwa. Anawakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kuihifadhi imani, na kuwaeleza kuwa Kristo alikuja katika mwili.MwandishiMtume Yohana.KusudiYohana anaonesha wazi kuwa Yesu ni Mungu aliyefanyika mwili, na hivyo kupinga kabisa ile dhana kwamba Kristo aliwaziwa tu kama aliyekuwa na mwili, eti kwamba yeye alikuwa roho.MahaliEfeso.TareheMnamo 85–90 B.K.Wahusika WakuuYohana na Yesu.Wazo KuuSi jambo gumu kupingana na mafundisho yanayokataa wazi misingi ya imani. Lakini mawazo potovu yanayofanana na kweli ya Injili yanapoingia, basi hili linakuwa tatizo kubwa.Mambo MuhimuMwana wa Mungu alikuja ulimwenguni katika mwili, alisikika na watu, alionekana, aligusika na walimkazia macho. Waraka huu unatangaza imani ya kweli katika Kristo ni imani katika Mungu kufanyika mwili, na maisha ya Kikristo ni upendano wa ndugu.YaliyomoUtangulizi (1:1‑4)Maisha ya Mkristo (1:5–2:29)Upendo wa kweli (3:1-24)Imani na kuona kwa hakika (4:1–5:21).