1Wale wamtumainio Bwana ni kama Mlima Sayuni,
ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.
2Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,
ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake
sasa na hata milele.
3Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi
waliyopewa wenye haki,
ili wenye haki wasije wakatumia
mikono yao kutenda ubaya.
4Ee Bwana, watendee mema walio wema,
wale walio wanyofu wa moyo.
5Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,
Bwana atawafukuza pamoja na watenda maovu.
Amani iwe juu ya Israeli.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.