Zaburi 52 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 52Hukumu ya MunguKwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi ameenda nyumbani mwa Ahimeleki.”

1Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya?

Kwa nini unajivuna mchana kutwa,

wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?

2Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.

Ni kama wembe mkali, ninyi mnaofanya hila.

3Unapenda mabaya kuliko mema,

uongo kuliko kusema kweli.

4Unapenda kila neno lenye kudhuru,

ewe ulimi wenye hila!

5Hakika Mungu atakushusha chini

kwa maangamizi ya milele:

atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu

kutoka hema lako,

atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.

6Wenye haki wataona na kuogopa;

watamcheka, wakisema,

7“Huyu ni yule mtu ambaye

hakumfanya Mungu kuwa ngome yake,

bali alitumainia wingi wa utajiri wake,

na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

Neema ya Mungu

8Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni

unaostawi katika nyumba ya Mungu,

nautegemea upendo wa Mungu usiokoma

milele na milele.

9Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda,

nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema.

Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help