Hagai Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziHagai ni moja ya vitabu vitatu vya kinabii vya Agano la Kale vilivyoandikwa baada ya Wayahudi kurudi nyumbani kutoka uhamishoni Babeli. Baada ya Mfalme Dario kutoa amri ya kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu kutoka uhamishoni, Hagai na Zekaria waliwatia moyo watu hao kulijenga upya Hekalu la Bwana.Kundi la kwanza la Wayahudi liliporudi Yerusalemu liliweka msingi wa Hekalu jipya kwa furaha na matumaini makubwa. Hata hivyo, Wasamaria na majirani wengine walipinga ujenzi huo kwa nguvu nyingi na kuwakatisha tamaa wafanyakazi, na kusababisha ujenzi huo usimame. Watu wakageukia ujenzi wa nyumba zao wenyewe. Nabii Hagai aliwahimiza watu kwamba ulikuwa wakati wa kuanza kujenga upya nyumba ya Mungu.MwandishiHagai.KusudiKujenga upya Hekalu la Mungu.MahaliYerusalemu.TareheMnamo 520 K.K.Wahusika WakuuHagai, Zerubabeli, Yoshua.Wazo KuuHagai aliwaambia watu kwamba utukufu wa Hekalu walilokuwa wanajenga ungekuwa mkubwa kuliko ule wa Hekalu lililotangulia, ingawaje halingekuwa imara kama la kwanza. Hili Hekalu lingekuwa bora zaidi kwa sababu Mungu angelijaza utukufu wake ndani yake.Mambo MuhimuKuwaita watu kujenga upya Hekalu huko Yerusalemu lililokuwa limebomolewa, na ahadi ya Mungu ya kuwabariki kama wangemtii.YaliyomoWito wa kujenga Hekalu (1:1‑15)Matumaini ya Hekalu jipya, na baraka zilizoahidiwa (2:1‑23).