Zaburi 4 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 4Sala ya jioni ya kuomba msaadaKwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi.

1Nijibu nikuitapo,

Ee Mungu wangu mwenye haki!

Nipumzishe katika shida zangu;

nirehemu, usikie ombi langu.

2Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu

kuwa aibu hadi lini?

Mtapenda udanganyifu

na kufuata miungu ya uongo hadi lini?

3Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga

wale wamchao kwa ajili yake;

Bwana atanisikia nimwitapo.

4Katika hasira yako, usitende dhambi.

Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu,

mkiichunguza mioyo yenu.

5Toeni dhabihu zilizo haki;

mtegemeeni Bwana.

6Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye

kutuonesha jema lolote?”

Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako.

7Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa

kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.

8Nitajilaza chini na kulala kwa amani,

kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana,

waniwezesha kukaa kwa salama.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help