1 Pet 3 - Swahili Union Version Bible

Wake na Waume

1 Efe 5:22; Kol 3:18; Tit 2:5 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

21 Pet 2:12wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.

31 Tim 2:9; Isa 3:18-24Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

4bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

5Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

6Mwa 18:12; Mit 3:25Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.

7Efe 5:25; Kol 3:19Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Mateso kwa ajili ya Kutenda Haki

8 Rum 12:16 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;

9Zab 34:12-16; Yak 1:26; Mt 5:44; 1 The 5:15; 1 Pet 2:23watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

10Zab 34:12-16; Yak 1:26Kwa maana,

Atakaye kupenda maisha,

Na kuona siku njema,

Auzuie ulimi wake usinene mabaya,

Na midomo yake isiseme hila.

11Na aache mabaya, atende mema;

Atafute amani, aifuate sana.

12Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,

Na masikio yake husikiliza maombi yao;

Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.

13Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?

14Mt 5:10; Isa 8:12-13; 1 Pet 2:20Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.

15Isa 8:13; 1 Pet 1:3,13Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.

161 Pet 2:12Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.

171 Pet 2:20-24Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.

18Rum 6:10; Efe 2:18; Ebr 9:28; 10:10Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,

191 Pet 4:8ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;

20Mwa 6:1—7:7,17,24watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.

21Efe 5:26; Ebr 10:22Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.

22Efe 1:20,21; Zab 110:1; Kol 1:16Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help